JINSI YA KUTENGENEZA TOMATO SAUCE:






MAHITAJI YA KUTENGENEZA TOMATO SAUCE

Nyanya kilo moja
2.   Vitunguu viwili
3.   Vinegar vijiko vitatu vya chai
4.   Sukari vijiko viwili vya chai
5.   Sodium Benzoate nusu kijiko cha chai
6.   Chumvi kijiko kimoja cha chai
7.   Maji ya moto kikombe kimoja cha chai
8.   Mafuta ya kula yasiyoganda vijiko saba vya kula 


JINSI YA KUANDAA NA KUITAYARISHA TOMATO SOURCE:          
1.   Osha nyanya na vitunguu kwa maji safi na salama
2.   Menya nyanya na vitunguu kisha kata vipande vidogovidogo
3.   Weka malighafi kuanzia namba moja mpaka namba nne katika blenda kulingana na uwiano hapo juu na saga kwa dakika kadhaa mpaka uone rojo laini.
4.   Weka sufuria jikoni na weka mafuta ya kula na uache yachemke
5.   Mimina mseto kisha uanze kukoroga kwa dakika 30 kuelekea upande mmoja
6.   Baada ya hapo ipua mseto na utakuwa tayari kwa kufungasha
7.   Weka kwenye chupa na bandika lebo
8.   Peleka  sokoni