INTER PRENUORSHIP LESSONS.



Kabla ya kusindika vitunguu saumu ni muhimu kuhakikisha kuwa vitunguu vinavyosindikwa vimekomaa vizuri na vipo kwenye kiwango cha ubora na havijaoza.


DALILI ZA VITUNGUU SAUMU VILIVYOKOMAA

1.   Vitunguu saumu huwa tayari kuvunwa katika kipindi cha miezi mitatu hadi mitano tangu kusia Mbegu


2.   Vitunguu saumu vilivyokomaa huonyesha majani kunyauka na kubadilika rangi na kuwa ya manjano hadi kahawia.


3.   Shingo ya vitunguu saumu hulegea na majani yake huanguka.


BIDHAA ZITOKANAZO NA KUSINDIKA VITUNGUU SAUMU

Kitunguu saumu huweza kusindikwa ili kuongeza thamani kwa kuzalisha bidhaa ambazo ni pesti pamoja na unga.


KUSINDIKA KITUNGUU SAUMU ILI KUPATA PESTI (LAHAMU)

Kuna njia mbalimbali za kutengeneza lahamu ya vitunguu saumu, lahamu nyingine huchanganywa na viungo, na nyingine hutumia vitunguu saumu ambavyo vimepikwa kidogo. Vifaa kwa ajili ya kusindika ni pamoja na kisu kikali kisichoshika kutu, meza safi yenye kufunikwa na bati la aluminiamu, chupa zenye mifuniko imara, mashine ndogo ya kusaga vitunguu saumu, jiko, sufuria, lebo, lakiri na mizani. Malighafi ni pamoja na vitunguu saumu, maji safi, chumvi, siki au sodiamu benzoate na mafuta ya maji.


JINSI YA KUSINDIKA

1.   Chagua vitunguu saumu ambavyo havina ukungu na mikwaruzo na ondoa magamba kwa kutumia kisu.


2.   Ondoa vikonyo vyote na menya kisha osha kwa maji safi na salama.


3.   Weka vitunguu saumu safi vilivyomenywa kwenye sufuria ya maji safi yanayochemka kwa muda wa dakika moja.


4.   Ondoa kwenye maji na saga kwa kutumia mashine kisha pima uzito wa pesti.


5.   Ongeza chumvi asilimia 5, yaani gramu 50 kwa kila kilo moja ya pesti.


6.   Ongeza ndimu au siki maalumu (balsamic vinegar) gramu 30 kwa kila kilo moja ya pesti.


7.    Ongeza mafuta ya maji kiasi cha gramu 30 kwa kila kilo moja ya pesti. Hii husaidia vitunguu kuhifadhiwa kwa muda mrefu.


8.   Koroga mchanganyiko hadi uwiane na fungasha kwenye chupa safi zilizochemshwa.


9.   Panga chupa kwenye sufuria kisha weka maji hadi yafikie nusu kimo cha chupa hizo na chemsha kwenye moto wa kadiri kwa muda wa dakika 25 hadi 30.


10.  Ipua, acha zipoe kisha weka lebo na lakiri.


11.  Hifadhi sehemu yenye ubaridi, kavu na yenye mwanga uliofifia.


12.  Vitunguu saumu vilivyosindikwa vizuri huweza kuhifadhiwa kwa zaidi ya miezi sita katika hali ya kawaida bila kuharibika.


MATUMIZI YA PESTI YA VITUNGUU SAUMU

Pesti ya vitunguu saumu hutumika kama kiungo katika vyakula mbalimbali, dawa ya kutuliza magonjwa na kuzuia magonjwa mengine.


KUSINDIKA VITUNGUU SAUMU KUPATA UNGA

Vifaa vinavyohitajika ni pamoja na kaushio bora, mashine ya kusaga, kisu kisichoshika kutu, chekeche, mabeseni na chupa za kuweka viungo. Maligafi ni vitunguu safi visivyokuwa na ukungu.


JINSI YA KUTENGENEZA

1.   Chagua vitunguu saumu ambavyo havina ukungu wala magonjwa na menya kwa kutumia kisu kisichoshika kutu.


2.   Osha kwa maji safi na salama kisha katakata vipande vidogovisivyozidi unene wa milimita 2.


3.   Kausha kwa kutumia kaushio au kichanja bora kisha saga kwa kutumia mashine ili kupata unga.


4.   Chekecha unga huo ili kupata unga laini na fungasha kwenye chupa safi zilizochemshwa na funga kwa mifuniko.


5.   Weka lakiri na lebo kisha hifadhi sehemu iliyo baridi, kavu na yenye mwanga hafifu.



MATUMIZI YA UNGA WA VITUNGUU SAUMU

Hutumika kama kiungo katika vyakula mbalimbali kama ambavyo kitunguu saumu kibichi inavyotwangwa na kutumiwa.


UTENGENEZAJI WA ACHALI YA EMBE:
Mango pickle ni moja kati ya bidha zinazoleta hamu ya kula kwa baadhi ya watu kwa kua ina ladha ya uchachi kidogo na pilipili kwa mbali. Hivyo hufanya baadhi ya watu kuitumia wakati wa kula chakula ili kupata ladha nzuri zaidi ya chakula.
  SAID NGUZO
                                                                  










   MANGO PICKLE ZINAZOZALISHWA NA
            MWANDISHI WA MAKALA HII

MALI GHAFI:                                             
1.   Embe
2.   Sukari
3.   Pilipili nyekundu
4.   Haladali
5.   Uwatu
6.   Siki/Vinegar                                                           
7.   Mafuta ya Alizeti/Mafuta yasiyoganda

VIFAA VITAKAVYOTUMIKA:                           
1.   Ndoo ya plastiki
2.   Sufuria kubwa
3.   Dishi la plastiki
4.   Sufuria ndogo
5.   Mwiko kwa ajili ya kukorogea
6.   Brush
7.   Visu visivyoshika kutu
8.   Jiko
9.   Meza yenye bati la aluminium
10.    Mzani
11.    Kinu au blender

HATUA ZA UVUMBIKAJI:
1.   Osha embe kwa maji safi yaliyochemshwa na kupoa
2.   Katakata embe bila kumenya vipande vidogo kwa kisu kisichoshika kutu
3.   Weka chumvi kulingana na kiasi cha embe ulichopata, mfano:
Kilo 20 za embe changanya na kilo tatu za chumvi. (changanya vizuri)
4.   Weka kwenye jaba au ndoo na funga vizuri, Hakikisha hewa haiingii halafu hifadhi sehemu salama
5.   Acha kwa wiki nne mpaka sita, lakini kila wiki tazama chumvi kama badi ni ya kutosha. Kama haitohi basi ongeza kilo moja kwenye kilo kumi.

ZINGATIA:
Embe hii iliyosindikwa hukaa kwa muda wa miaka mitatu mpaka mitano.

UTENGENEZAJI WA ACHALI SASA BAADA YA UVUMBIKAJI WA EMBE
1.   Osha embe mara tatu kwa maji safi yaliyochemshwa na kupoa ili kuondoa chumvi
2.   Weka kwenye chujio kwa masaa 24 (siku nzima) ili kuchuja maji.
3.   Pima uzito ili uweze kujua kipimo ikusaidie katika uchanganyaji na malighafi nyingine
                                  
KUCHANGANYA:
1.   Ndoo ndogo (lita kumi)
a.   Uwatu uliokaangwa na kusagwa vijiko sita vya chakula
b.   Haladali iliyokaangwa na kusagwa vijiko vitatu vya chakula
c.   Sukari vijiko vitatu vya chakula
d.   Pilipili nyekundu robo kilo

2.   Changanya na koroga kupata mchanganyiko mzuri
3.   Weka siki chupa tatu/lita tatu
4.   Weka mafuta ya kula kikombe kimoja kile kidogo cha ndani cha chupa ya chai.
5.   Funika kwa dakika kumi
6.   Funua na koroga kupata mchanganyiko.
7.   Weka kwenye vifungashio, ongeza mafuta ya kula kidogo juu ya kifungashio na funga weka lebo
8.   Peleka sokoni
N:B:
Mafuta ya kula unayotumia ni lazima yawe yamechemshwa na kupoa


Kwa maswali, maoni au ushauri juu ya utengenezaji wa Mango pickle wasiliana na mwandishi wa makala hii kwa simu namba 0758 216548, 0713 330280 au